about us
about us
Kuhusu Sisi
Sisi ni Nani?
Chuo cha Africa Academy ni jukwaa maalum la kwanza la Kiislamu, la bure na la kimtandao lenye lengo la kuwasaidia wazungumzaji wa Kiswahili kufikia uelewa sahihi wa Uislamu kupitia Qur’an Tukufu na Sunnah za Mtume Muhammad ﷺ.
Ni jukwaa la kimtandao linalofanya kazi mtandaoni kwa 100%, likileta watu karibu na maarifa ya Kiislamu kupitia intaneti, mitandao ya kijamii na chaneli za Afrika TV — kwa mfumo wa elimu huria wa kozi fupi (MOOCs – Massive Open Online Courses), na masomo ya kielektroniki shirikishi. Linategemea walimu mahiri na maarufu kutoka miongoni mwa wahubiri wa Ahlus-Sunna wal-Jama’a wanaozungumza Kiswahili.
Dhamira na Maono Yetu
Dhamira
Africa Academy iwe taasisi ya kielimu inayoongoza katika elimu ya kupitia mtandao kwa lugha ya Kiswahili, kwa kutumia mbinu za kisasa na teknolojia bora, kupitia matangazo ya televisheni ya satelaiti na majukwaa mbalimbali ya intaneti.
Maono
Tunatarajia katika awamu tatu za kwanza kushirikisha wanufaika 30,000 kupitia mfumo wetu wa elimu huria.
Malengo yetu
Kukidhi haja ya Waislamu juu ya misingi ya maarifa ya Kiislamu na kile ambacho mtafutaji wa elimu hapaswi kutokujua, kwa lugha za Kiafrika.
Kueneza itikadi ya Ahl al-Sunnah wal-Jama’ah na Fiqh sahihi kwa ushahidi wake kutoka kwa Qur’an na Sunnah.
Kumfundisha wanamke wa Kiislamu dini yao, kuongeza uelewa wao na kuchangia katika maandalizi ya wanafunzi wa kike wa elimu ya Kiislamu.
Kueneza utamaduni wa kujifunza elimu za Sharia kwa njia ya mtandao barani Afrika kwa kutoa mtaala wa kielimu unaozingatia utaalamu na uvumbuzi katika mbinu za uwasilishaji.